Mashariki mwa DRC: Raia waelezea masaibu wanayoyapata kufuatia ukatili wa ADF
Mashambulizi ya ADF, kundi lenye silaha lenye asili ya Uganda lenye uhusiano na Dola la Kiislamu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yanaendelea. Mapema mwezi Machi, mashambulizi mawili mfululizo katika eneo la Mambasa la mkoa wa Ituri yalisababisha watu wengi kuhama makazi yao na kukimbilia Bafwasende na hadi Kisangani, katika mkoa jirani wa Tshopo.
2026-03-22 05:46:26